Local Bulletins

Wananchi wa Manyatta Ginda, Marsabit walalamikia ubovu wa barabara unaotajwa kulemaza upatikanaji wa huduma muhimu.

Na JB Nateleng

Wakazi wa Manyatta Ginda, eneo bunge la Saku, kaunti ya Marsabit wamelalamikia ubovu wa barabara ambao wameitaja kuwa imelemeza upatikanaji wa huduma muhimu katika eneo hilo.

Wakazi hawa wamesema kuwa ubovu wa Barabara umewasabibisha watoto kutofika shuleni kwa wakati na hata wakati mwingine watoto wanakosa kuenda shule. Wameitaka serekali kuweza kuwarekebishia barabara haswa wakati huu ambapo mvua inatarajiwa kunyesha.

Akizungumza na idhaaa hii kwa niaba ya wakazi wa eneo Hilo Mzee Ali Roba amesema kuwa wamekuwa wakiwaelezea viongozi kuhusu matatizo ya barabara lakini wameyafumbia macho na kuwaaacha bila hata kufikiria kuukarabati barabara hiyo.

Subscribe to eNewsletter