Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Caroline Waforo,
Wananchi katika lokesheni ya Hurri Hills,eneo bunge la North Horr kaunti ya Marsabit wamekubali kutoa kipande cha ardhi cha ekari 200 kwa idara ya misutu jimboni kwa kipindi cha miaka 10, kitakachotumika katika mradi wa kuimarisha ardhi na kiwango cha misitu ambapo miche millioni 2 itapandwa katika kipande hicho cha ardhi.
Haya yalibainika wakati wa kikao cha siku ya Jumanne cha kuhamasisha jamii ya eneo hilo kuhusiana na umuhimu wa mradi huo utakao tekelezwa katika kaunti za Marsabit, Samburu pamoja na kaunti ya Wajir,kilichoongozwa na idara ya misutu jimboni na kuwashirikisha waakilishi wa makundi mbalimbali katika eneo hilo.
Akizungumza na wanahabari mhifadhi wa msitu wa Marsabit Mark Lenguro amesema kuwa mradi huo wa kuimarisha ardhi na kiwango cha misitu katika kaunti hizo tatu utagharimu kitita cha shilingi bilioni 74 na utaanza kutekelezwa katika kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2025/2026.
Mradi huo pia utafanyika katika maeneo bunge ya Saku na Laisamis.
Kulingana na mhifadhi huyo wa misutu mradi huu utasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo wakaazi wa eneo hilo wanapitia ikiwemo ukosefu wa maji.
Kwa upande wake Boniface Wario aliyezungumza kwa niaba ya jamii hiyo,amesema kuwa mradi huo utakuwa wa manufaa kwao pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huu ni wa kipindi cha miaka mitano. Baadae jamii inaweza kuongeza muda zaidi wa makubaliano hayo japo jamii ya Hurri Hills imetoa ardhi kwa kipindi cha miaka 10.
Baada ya muda wa makubaliano hayo kutamatika idara ya misitu inarejesha ardhi hiyo kwa jamii.
Iwapo mradi huo utatekelezwa utasaidia pakubwa katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kufanikisha mpango wa serikali ya Kenya ya kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032.