Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Caroline Waforo
Wanafunzi wa shule za upili na haswa walio katika shule za kutwa wameshauriwa kukoma kujihusisha na mapenzi.
Wito huu umetolewa na mkurugenzi wa shirika la Wongan Women Initiative Teresalba Sintian ambaye amezungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu.
Teresalba amewataka wanafunzi kujenga maisha yao ya usoni na kutambua kuwa kila kitu kina wakati wake.
Na huku ripoti ikiashiria kuwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wanatumia dawa za kulevya pamoja na mihadarati Teresalba ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuwajibika katika malezi ya wanao ili kuwaepusha na matumizi wa dawa hizo.
Majuma kadhaa yaliyopita mamlaka ya kupambana na utumizi wa dawa za kulevya nchini NACADA ilitoa ripoti iliyoashiria kuwa asilimia 45% ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni waraibu wa dawa za kulevya.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa kuwa zaidi ya asilimia 8 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni waraibu wa mihadarati na wanafaa kusajiliwa katika vituo vya ubadilisha tabia.
Pombe ilitajwa kutumika sana vyuoni kwa ailimia 40.5, sigara 13.4% na kisha shisha kwa asilimia 10.9