KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Joseph Muchai,
Wiki chache baada ya serikali kuu kupitia wizara ya elimu kutangaza kuwa wanafunzi walikamilisha elimu na hawajapokea vyeti vyao kutokana na kushindwa kukamilisha karo kupokezwa vyeti hivyo bila ada yeyote, bado agizo hilo halijakuwa likitekelezwa mashinani na huenda ikachukua muda zaidi kwa wanafunzi hao kupata vyeti vyao.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa wangali wanangojea maelekezo rasmi kutoka kwa wizara ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi hao kupata vyeti vyao.
Akiongea na idhaa hii baada ya mkutano kati ya wizara ya elimu, baraza la mitihani nchini KNEC, walimu wakuu pamoja na washikadau wengine katika idara ya elimu jimboni Marsabit uliofanyika katika shule ya upili ya Moi Girls Magiri aidha amesema kuwa barua kutoka kwa wizara itawawedzesha utekelezwaji wa agizo hilo la waziri.
Sasa Magiri anawataka wanafunzi hao kuwa na subira huku swala hilo likiendelea kushughulikiwa.
Haya yanajiri huku kukiwa na vuta nikuvute baina ya wanafunzi hao wa zamani na baadhi ya walimu wakuu wa shule walizosomea wakidai kuwa walimu wakuu wanakaidi amri ya wizara ya elimu ya kutoa vyeti hivyo bila ada yeyote.