Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Shirika la Friends of Lake Turkana (FoLT) linaandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa kamati za mabadiliko ya tabia nchini kutoka wadi mbalimbali za jimbo la Marsabit.
Kwa mujibu wa afisa katika shirika la Friends of Lake Turkana Dismus Achila ni kuwa zoezi hili linalenga kutoa hamasa kwa wanachama hao ili kuhakikisha kwamba vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchini inafaulu katika kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani, Achilla amesema kuwa warsha hiyo inalenga kuwapa hamasa zaidi wanachama wa kamati hizo kuhusiana na namna wanaovyeweza kuendeleza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mashinani.
Aidha Achila amesema kuwa warsha hiyo pia itahakikisha kwamba wanachama wanajibiwa maswali kuhusiana na namna sera zinavyoweza boreshwa ili kupiga jeki vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha baadhi ya wanachama wa kamati hizo wamelalamikia kile wamekitaja ni kulemazwa kwa juhudi za kuimarisha vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka kwa viongozi.