Local Bulletins

Wana-loiyangalani wataadharishwa dhidi ya mafuriko inayotokana na mvua

Na JB Nateleng

Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa eneo la Loiyangalani eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa naibu kamishna wa Loiyangalani Stanley Kimanga ni kwamba eneo hilo limeweza kupekea mvua kubwa sana ambayo imenyesha kutoka asubuhi mpaka jioni akiwataka wakazi kuchukua tahadhari ya kutovuka ama kutembea kuliko na maji mengi.

Akizungumza na shajara kwa njia ya simu, Kimanga amesema kuwa bado hawajabainisha idadi kamili ya mifugo au mali iliyoharibiwa na mvua hiyo huku akisema kuwa serekali iko imara na tayari kukabiliana na mathara yoyote yatakayotokana na mvua hiyo.

 

Subscribe to eNewsletter