Local Bulletins

Wamiliki wa majengo yaliyo na mabati ya Asbesto watawajibika kwa gharama ya kuyaondoa kwa majengo yao.

Na JB Nateleng

Wamiliki wa majengo yaliyo na mabati ya Asbestos watawajibikia gharama ya kuyaondoa paa hizo kwenye majengo na nyumba zao.

Hii ni kufuatia agizo la Baraza la Mawaziri kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira nchini (NEMA) kusimamia kuondolewa wa mabati hayo ambayo yamekisiwa kuwa yanaweza kusababisha saratani.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa NEMA tawi la Marsabit Naftali Osoro ni kwamba wametambua vituo 9 ambavyo vimetumia mabati ya Asbestos huku akisema kuwa wanafuatilia ili kuhakikisha kuwa wameyaondoa kwa njia inayofaa ili kulinda mazingira na watu kwa ujumla.

Osoro amevitaka vituo hivyo kuchukua leseni kwa NEMA kabla ya kuanza mchakato wa kutoa mabati hayo.

Mkurugenzi huyu amesema kuwa watashirikiana na serekali ya kaunti ya Marsabit ili kutambua eneo salama ambamo watazikia mabati haya kwa manufaa ya kulinda mazingira na wakazi.

Aidha ameelezea kuwa mabati ya Asbestos lazima yafukiwe chini ya mchanga kwa njia inayofaa ili kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji wakati mvua inaponyesha.

Osoro hata hivo ametoa tahadhari kwa wakazi wa Marsabit kutotumia  mabati ya Asbestos akisema kuwa ni hatari na huenda ikaathiri afya yao.

Subscribe to eNewsletter