Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Isaac Waihenya,
Warsha ya siku mbili ya kuwapa mafunzo ya kidijitali walimu wa shule za msingi na msingi sekondari (JSS) katika kaunti ya Marsabit imekamilika huku wito wa kuongeza idadi ya shule zinazonufaika na mpango huo ukisheni.
Akuzungumza wakti wa kufunga warsha hiyo mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri, amewataka walimu waliopata mafunzo hayo kuyatumia kuwaimarisha wanafunzi kidijitali.
Magiri amewataka walimu waliopata mafunzo hayo pia kuhakikisha kwamba vifaa vya masomo vilivyotolewa na serekali kuendeleza mafunzo ya kidijitali vitatumika vyema shuleni.
Aidha baadhi ya walimu waliohudhuria hafla hiyo wametaja hoja ya mafunzo ya kidijitali kutiiliwa maanani kwani eneo hili limebaki nyuma ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchini.
Vilevile wametoa wito wa idadi ya shule ambazo zinapata mafunzo hayo kuongezwa, ili kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi katika kaunti ya Marsabit wamepata ujuzi wa kidijitali.
Warsha hii iIiyofadhiliwa na shirika la Raspberry Pi Foundation na kutekelezwa na Baraza la maendeleo la kaunti zilizopo maeneo kame (FCDC) ililenga kuwapa mafunzo ya kidijidali walimu 15 kutoka shule 12 za maeneo bunge yote manne ya kaunti ya Marsabit kama njia moja wapo ya kupiga jeki mtaala mpya wa elimu (CBE).
Mradi huu unatekelezwa katika kaunti 10 kaunti zilizopo maeneo kame (FCDC) ambazo ni Marsabit Turkana, West Pokot, Lamu, Wajir, Isiolo, Tana River, Samburu, Garissa, na Mandera.