Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Sabalua Moses
Wakulima kaunti ya Marsabit wamenufaika na mradi wa kaunti kupitia idara ya kilimo pamoja na shirika la chakula ulimwenguni WFP ya kuwapa mafunzo pamoja na vyandarua vya kustahimili makali ya jua yaani shade nets.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani mjini Marsabit kaimu mkuu katika idara ya ukulima Wako Denge Halake amesema kuwa vifaa hivyo vimeweza kusaidia wakulima sitini katika kaunti hii pamoja na mafunzo ili kuboresha ukulima pamoja na kukuza ukulima endelevu.
Vile vile, Wako amesema kuwa vyandarua hivyo kwa vitasaidia wakulima kukabiliana na makali ya jua pamoja na mabdiliko ya tabia nchi kaunti ya Marsabit.
Wakati huo huo Wako amewahimiza wakulima kupanda mimea ambayo inaweza kustahamili ukame haswa wakati huu wa mvua