Local Bulletins

Wakristu wa kanisa Katoliki wajiandaa kuanza msimu wa Kwaresma kesho siku ya Jumatano ya majivu.

Na Henry Khoyan

Huku ikiwa imebakia siku moja tu kabla ya Siku ya Jumatano ya Majivu, waumini wa Kanisa la Kikatoliki katika Jimbo la Marsabit wamejiandaa kwa sherehe za kipekee zitakazofanyika kesho Jumatano.

Siku ya Majivu ni mwanzo wa Kipindi cha Kwaresima, kipindi cha siku 40 ya kufanya toba (yaani kutubu) na maandalizi ya kiroho kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka,Waumini wamehimizwa kujitafakari, kuombea toba, na kufanya matendo mema.

Padre Abraham Ali anahudumu katika parokia ya cathedral mjini Marsabit na anaeleza Zaidi.

Fr. Abraham Ali amesisitiza umuhimu wa kuonyesha ukarimu na kujali wasiojiweza.

Amewahimiza wakristu wawe mfano bora kwa kufuata mafundisho ya kanisa, kiroho na kuchukua hatua madhubuti za kusaidia wale wanaohitaji.

Ametoa wito kwa wakristu jimboni kuacha maisha ya dhambi na kumkaribia Mungu kwani wanapojitenga na dhambi na kuelekeza mioyo yao kwa Mungu, watapata amani, furaha na mwongozo katika maisha yao.

Subscribe to eNewsletter