Local Bulletins

Wakristo jimboni Marsabit watakiwa kujitolea kuwasaidia waisojiweza msimu huu wa Kwaresma.

Na JB Nateleng,

Msimu wa Kwaresma ni msimu wa kujitolea kuwasaidia wasiojiweza katika jamii kwa kuwatembelea na kusali nao.

Haya ni kwa mujibu wa mtawa Mourine kutoka shirika la St Teresa Charity Sister, hapa jimboni Marsabit.

Mtawa Mourine amesema kuwa lazima tuangalie katika jamii wale wasiojiweza na tuwasaidie ili nao waweze kuhisi uwepo wa Mungu ndani yao.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee mtawa Mourine amesema kuwa ni wajibu wa kila Mkristo kukumbuka jirani na kufanya tendo ambao linaweza msaidia msimu huu wa Kwaresma.

Pia mtawa Mourine amewarai Wakristo kuweza kudumu katika sala msimu huu wa Kwaresma ili kuweza kujua na kutambua mpango wake Mungu katika maisha ya Wakristo.

Kadhalika mtawa huyu amewataka Wakristo kuweza kuyazingatia mafundisho wanayofundishwa kanisani ili kuimarisha Imani yao na kuacha kuyumba yumba kiimani.

Subscribe to eNewsletter