Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
WAKULIMA na wafugaji katika eneo la Songa, eneobunge la Saku kaunti ya Marsabit wameonesha hofu ya kutokana na utabiri kuwa huenda Marsabit ikapokea kiasi kidogo sana ya mvua msimu wa mwezi wa Tatu, Nne na Tano.
Wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na Soba Liaro wamesema kuwa kutokana na wao kuwa wakulima – utabiri wa idara ya hali ya hewa kuwa mvua kidogo huenda ikanyesha itawaumiza sana kwani msimu jana pia hawakuvuna chochote kutokana na mvua kunyesha kwa muda mfupi.
Liaro akizungumza na kituo hiki katika eneo la Songa amesema kuwa serikali zote mbili zina wajibu wa kusaidia wafugaji kulipa au kupunguza karo ya shule kwani kitega uchumi chao hakipo kwa sasa kutokana mifugo mingi kufa au kuibiwa na wezi.
Anasema kuwa mifungo kupungua kupitia wizi na hata mabadiliko ya Tabianchi imewarudisha nyuma na sasa wanairai mbunge wao kuwakumbuka wanapogawanya pesa za basari ili kuzuia wanafunzi kutumwa nyumbani.
Wakati huo wameitaka serikali kuu ama ya kaunti kuwarekebishia barabara ya kutoka songa kwenda mjini marsabit kutokana na barabara mbaya isiyopitika haswa pindi inaponyesha mvua hatua wanayosema hutatiza usafirishaji wa mavuno yao kwenda mjini.