NA JBNateleng
Wakazi wa manyatta Boqe wadi ya Maikona eneo bunge la North Horr kaunti ya Marsabit wamelalamikia uhaba wa maji kufuatia kuharibika kwa bwawa la Laq Lokho.
Wakizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, wakazi hao wamedai kuwa wamekumbwa na changamoto ya maji tangu bwawa hilo liharibike mwaka moja uliopita.
Luka Kulula ambaye ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa uhaba wa maji katika eneo hilo umesambaratisha afya pamoja na elimu kwa sababu watu wengi wameamua kuyaacha makazi yao na kuenda kusaka maji jambo ambalo linalemaza pia maendeleo katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa bwawa hilo Boya Sharamo amesema kuwa juhudi zao za kusaka usaidizi kutoka kwa serekali zimeambulia patupu huku akidai kuwa hata maji wanayopata kupitia malori ya maji bado hayatoshi kukimu mahitaji yao ya kila siku.
Wakazi hawa wametoa wito kwa idara ya maji jimboni Marsabit kuweza kuzuru eneo hilo na kutathmini uhalisia wa uhaba wa maji katika bwawa hilo ili kutoa suluhu ya kudumu.
Wanandoa wametakiwa kujua hali yao ya afya ili kujenga familia imara na dhabiti.