Local Bulletins

Wakazi mjini Marsabit watoa hisia tofauti kutokana na serikali kutaka kuweka CCTV katika kila kituo cha polisi.

Na Sabalua Moses

Kufuatia serikali kutaka kuweka CCTV katika vituo vyote humu nchini wakazi mjini Marsabit wametoa hisia mseto kuhusiana na matamshi yake waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen.

Haya yanajiri baada ya kifo cha aliyekuwa bloga Albert ojwang kuleta utatanishi na kuibua maswali katika idara ya polisi  katika utendakazi wao huku ikibainika kuwa baadhi ya video yaliondolewa katika kituo cha central police mjini Nairobi.

Wakenya wakizidi kutoa hisia tofauti, mjini Marsabit baadhi yao wametoa maoni   na kusema kuwa CCTV hizo  hazitasaidia kwani polisi wanaweza kuivuruga pia.

Vile vile baadhi yao wamesema kuwa ni njama ya serikali kutaka kutenga pesa katika miradi ambayo hayana manufaa katika idara hiyo ya polisi.

Hata hivyo wengine wao wamesema kuwekwa kwa CCTV katika vituo vya polisi kutasaidia kupunguza uhalifu katika idara ya polisi.

Subscribe to eNewsletter