Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATAKIWA KUJIANDAA KWA MVUA FUPI MSIMU HUU.

Marsabit- Muchai

Wakaazi wa Marsabit wametakiwa kujiandaa kwa mvua fupi msimu huu wa mwezi Machi, Aprili na May.

Kwa sasa hali ya ukame inaonekana kuwakodolea macho wakaazi haswa wafugaji kwani hali hiyo inasababisha uhaba wa maji na malisho.

Kaunti zinazotarajiwa kupata viwango vya chini vya mvua ni pamoja na baadhi ya maeneo ya  Garissa, Mandera, na Wajir

Nyingine ni Meru, Tharaka-Nithi, Embu, Kitui, Machakos, Makueni, Marsabit, and Isiolo.

Kulingana na ripoti kutoka idara ya hali ya anga maeneo ya kaskazini mwa nchi yanatarajiwa kupokea mvua ndogo ikilinganishwa sehemu nyingine za nchi ambazo zitapokea mvua nyingi na  za mapema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa idara hiyo Dkt David Gikungu, maeneo yanayotarajia mvua kwa wingi ni pamoja na Magharibi, Bonde la  Ziwa Victoria, Rift Valley, kati mwa Kenya (pamoja na Nairobi), Pwani, kusini mashariki na sehemu za Kaskazini. Walakini, mikoa mingine itapata hali ya hewa ya jua, ukavu na joto.

Joto la juu linatarajiwa kuwa zaidi ya nyuzi joto 30 wakati joto la chini litashuka chini ya nyuzi joto 10, haswa katika sehemu za Nyanda za Juu mashariki mwa Bonde la ufa, Kati na Kusini mwa Bonde ufa, na karibu na Mlima Kilimanjaro.

Mikoa inayozunguka Bonde la Ziwa Victoria na sehemu za Nyanda za Juu kwenye Bonde la Ufa zitapata vipindi vya jua wakati wa mchana lakini vinaweza pia kupata mvua za asubuhi na mvua za mchana.

Subscribe to eNewsletter