Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
WAKAAZI wa mji wa Marsabit wamefanya maadamano leo kulalamikia kifo cha Abraham Arbe mwanabodaboda aliyeuliwa kinyama katika eneo la Harobota nje kidogo wa mji wa Marsabit usiku wa Jumatatu.
Wakaazi hao wakizungumza na waandishi wa habari mjini Marsabit walipokua wakiandamana wakiwa wamebeba mwili wa marehemu, wameonesha masikitiko yao kutokana na kifo cha kijana huyo aliyekuwa akisaka riziki jioni.
Wakaazi hao pia wameshutumu idara ya usalama jimboni Marsabit haswa afisi ya kamishna wanaodai kuwa ilipuuza kilio chao cha kutafuta haki ya mwendazake.
MCA wa wadi ya Marsabit Central Jack Elisha amekemea kifo hicho akisema kuwa maisha ya kijana mdogo yamepotezwa na wahalifu kwa njia ya kinyama. Amemkosoa pia kamishna wa kaunti James Kamau kwa madai ya kutowasikiza waandamanaji.
Kauli yake imesisitizwa na MCA wa Heilu Manyatta Siba Aila.
Mwenyekiti wa kamati ya Amani katika bunge la Marsabit Tura Ruru ameomba wananchi wa Marsabit kutokubali kupiganishwa kwa msingi wa kikabila na wahalifu wachache.
Aliyekuwa mwaniaji wa ugavana mwaka wa 2022 Pius yattani pia amekashifu mauaji hayo huku akitaka wananchi kuipa fursa idara ya polisi kusaka wahalifu hao.
Wakati uo huo Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau akizungumza na waandishi wa habari ofisini mwake alisema kuwa kijana mwingine ameuawa akiwa malishoni katika eneo la dukana na idara ya usalama inafuatilia suala hilo.