photo courtesy
Local Bulletins

Wakaazi wa kaunti ya Marsabit watoa maoni mseto kuhusu siku 1000 za serikali ya Kenya Kwanza.

NA MUCHAI JOSEPH

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametoa maoni mseto kuhusu utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza siku 1001 tangu ilipochukua hatamu za uongozi. Wakiongea na Shajara Ya Radio Jangwani mjini Marsabit wakaazi hao ambao wengi ni wafanyibiashara wamesema kuwa serikali imekuwa ikitoa ahadi hewa na kusahau huduma kwa wananchi.

Baadhi wametaja utovu wa usalama kama swala tete kwenye uongozi wa serikali ya sasa. Utekaji nyara na ukatili wa polisi dhidi ya wananchi umeonekana kuwa kero sana kwa wananchi waliozungumza shajara.

Aidhaa baadhi wanahisi kuwa viongozi walioteuliwa wanafaa kujiuzulu haswa kutokana na mauaji yalioshuhudiwa hivi maajuzi dhidi ya mwana blogu Albert Ojwang.

Wakati uo huo baadhi yao wameeleza kuwa taasisi za umma zimepoteza uaminifu miongoni mwa wananchi.

Serikali ya Kenya Kwanza ilichukua hatamu za uongozi tarehe 13 septemba mwaka wa 2022 yapata siku 1001 hadi kufikia leo.

 

 

Subscribe to eNewsletter