Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Carol Waforo
Jamii zinazoishi katika kaunti ndogo ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit zimekubaliana kumaliza uhasama na kuishi kwa amani.
Hii ni kufuatia mkutano wa amani ulioandaliwa leo Jumatano na idara ya usalama katika eneo hilo na kuwaleta pamoja wazee kutoka jamii ya ELMOSARETU inayojumuisha jamii za Elmolo, Samburu, Rendile pamoja Turkana wanaoishi Loiyangalani.
Katika mkutano huo kamati ya amani imebuniwa ili kuhakikisha kuwa inaleta jamii hizo pamoja na kueeneza jumbe za amani.
Wakizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu baada ya kikao hicho wazee hao wamewataka wakaazi Loiyangalani kuishi kwa umoja.
Gideon Galoro ni mzee kutoka eneo hilo ambaye amesema wananchi ndio wana jukumu kuu la kuleta amani.
Katika mkutano huo jamii hizo zimekubaliana kwa pamoja kuwa zitatoa ripoti kwa idara ya usalama jimboni kuhusu matukio yoyote ya kiusalama katika eneo hilo.
Stephen Nakeno ni mzee kutoka eneo hilo na ambaye alikuwa mwakilishi wadi wa Loiyangalani.
Vijana pia wameendelea kutahadharishwa dhidi ya utumizi mitandao ya kijamii katika uchochezi.
Naftaly Kara ni Mmoja wa viongozi wa vijana katika eneo hilo.
Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Loiyangalani Stanley Kimanga kamati hiyo itahakikisha kuwa wageni wanaofika katika eneo la Loiyangalani wanatambulika ili kuzuia visa vya uhalifu pamoja na kuweka mikakati ya kuzuia mizozo ya maeneo ya malisho.
Siku ya Alhamisi baraza la amani litaandaliwa katika eneo lote na kuwaleta pamoja jamii zote zinazoishi katika eneo hilo.
Baraza hilo linatarajiwa kuongozwa na seneta wa kaunti ya Marsabit Mohammed Chute ambaye anatarajiwa kuandamana na viongozi wengine katika bunge la seneti.