Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wito umetolewa kwa wakaazi wa wadi ya Illeret hapa jimboni Marsabit kujitokeza ili kupata vitambulisho katika zoezi la usajili linaloendelea kwa sasa.
Kwa mujibu wa msajili wa watu katika kaunti ya Marsabit Isaac Kibet ni kuwa zoezi hilo la siku kumi limesimamiwa na katibu katika idara ya maeneo kame na ustawi wa miji Kello Harsama huku akiwataka waliomalishoni pia kutokea ili kupata stakabadhi hiyo muhimu.
Kibet aliyezungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee ametaja kwamba zoezi hilo limerahisishwa pia na kuondolewa kwa zoezi la kuwapiga watu msasa haswa walio katika maeneo yanayoapakana na mataifa jirani.
Aidha Kibet ametaja kwamba zoezi hilo linalenga kuhakisha kwamba waliosahaulika haswa waliopo mpakani wanapata vitambulisho huku wakilenga watu 5,000 katika zoezi hilo.
Kwa upande wake MCA wa wadi ya Illeret James Korie Haille amepongeza rais Wiliam Ruto kwa kuondoa zoezi la kuwapiga watu msasa sawa na katibu Kello Harsama aliyefanikisha zoezi hilo katika wadi hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walionufaika na zoezi hilo la utoaji vitabulisho wamepongeza serekali kuu na katibu Kello Harsama wakitaja kwamba litawaondolea mahangaiko waliokuwa wanapitia kutokana na kukosa kitambulisho.
Wakaazi wa eneo la Illeret wameishukuru idara ya maeneo kame na ustawi wa miji baada ya kupokea lori tatu cha chakula kutoka kwa idara hiyo.
Wakizungumza na Meza ya habari ya Radio Jangwani wakaazi hao wakiongozwa na Fauzia Silamo wametaja kufurahishwa na hatua ya serekali ya kitaifa kupitia katibu wa idara hiyo Kello Harsama kwa kuwakumbuka msimu huu wa ukame.
Wakaazi hao wamepokea magunia 900 ya mchele,magunia 720 ya maharagwe, magodoro 200, blanketi 500 pamoja na katoni 50 za sodo.
Kauli yao iliungwa mkono na MCA wa wadi hiyo James Korie Haille ambaye ameutaja msaada huo kama ambao umekuja wakati unafaa kutokana na kiangazi kinachoshuhudiwa eneo hilo, baada ya mvua chache kushuhudiwa mwaka jana.