Local Bulletins

WAKAAZI WA ENEO BUNGE LA SAKU WAJITOKEZA KUTOA MAONI KUHUSIANA NA MGOGORO UNAOZINGIRA NGCDF.

Na Henry Khoyan,

Wakaazi wa eneo bunge la Saku, Kaunti ya Marsabit, wameelezea kuunga mkono hazina ya maendeleo ya maeneo bunge (NGCDF) pamoja na hazina ya maendeleo ya akinamama na wakongwe (NGAFF) kuendelea kusimamiwa na wabunge.

Wakizungumza katika kikao cha kutoa maoni kilichoandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki hapa mjini Marsabit, baadhi ya yao wamesisitiza kuwa fedha hizo zinapaswa kubaki katika maeneo bunge na sio kwa serekali kuu.

Aidha wamelezea manufaa ambayo yemeletwa na fedha hizo ikiwemo kuwafadhili wanafunzi kutoka familia maskini kupata elimu.

Kwa upande wake Mbunge wa Saku, Ali Dido Raso, amesisitiza umuhimu wa fedha hizo kusalia kwa wabunge huku akiweka wazi kuwa asilimia 80 ya shule katika eneo bunge la Saku zinategemea fedha kutoka kwa hazina za NGCDF.

Mbunge huyo ameitaka serikali kuangazia masuala yaliyoibuliwa na pia kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kwa njia inayofaa.

Kauli yake Dido Ali Raso imekaririwa na mwakilishi wa wanawake hapa jimboni Marsabit Naomi Jillo Wako ambaye amezitaja fedha hizo kama zinazobadilisha maisha haswa ya watoto kutoka familia zisizojiweza.

Subscribe to eNewsletter