Local Bulletins

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit watoa maoni kuhusu bajeti ya mwaka wa kifedha 2025-2026.

Na Muchai Joseph

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametoa maoni yao mseto kuhusu bajeti ya mwaka wa kifedha 2025-2026. Wengi tuliosema nao wameonekana kupendelea bajeti ya mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliopita.

Wakizungumza na shajara ya redio jangwani wakaazi hawa wameelezea kuwa itakuwa vyema iwapo itatekelezwa kama ilivyo.

Hata hivyo wengine wanahisi kuwa bei ya bidhaa za mafuta imepanda kupita kiasi.

Hayo yakijiri baadhi wameelezea kuwa hawakupata nafasi ya kifuatilia makadirio ya bajeti kutokana na  maandamano yaliyokuwa yakiendelea jijini Nairobi. Wameelezea kuwa haki yake lazima ipatikane.

Subscribe to eNewsletter