Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
NA MOSES SABALUA
Wakaazi wa Marsabit wamehimizwa kukuza ufugaji wa nyuki kwani ina manufaa makubwa kwa jamii. Hayo ni kulingana naye Sisaye Bobgala ambaye ni mpatanishi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Inua Dada na mfugaji wa nyuki.
Akizungumza na kituo hiki mjini Marsabit Sisaye Bobgala amewataka haswa vijana wajiunge na ufugaji huo wakati huo ambapo kuna mabadiliko ya tabia nchi.
Vile vile Sisaye amesema ufugaji wa nyuki una faida mno na imeweza kukimu mahitaji ya wakulima wengi katika kaunti ya Marsabit.
Wakati huo huo amesema kuwa yupo tayari kukuza wakulima wachanga wanaotaka kujisaidia kuanza kuanza ufugaji wa nyuki.
.