Local Bulletins

Wakaazi jimboni Marsabit watakiwa kuishi kwa amani na kutumia rasilimali chache zilizopo kwa Amani.

Na Isaac Waihenya,
Wakaazi wa Marsabit la wametakiwa kuishi kwa amani na kutumia kwa pamoja rasilimali chache zilizopo katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa kamata wa polisi katika ukanda wa kaskazini mashariki Charles Naibei ni kuwa ipo haja ya jamii za Marsabit kukumbatia Amani na kuishi kwa pamoja.
Akizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Marsabit baada ya kuzuru maeneo ya Moyale, Sololo, Turbi,Balesaru, na Illeret katika kaunti ya Marsabit, Naibei ametaja kwamba ameandaa kikao na kamati mbalimbali za Amani katika maeneo hayona kuhimuza umuhimu wa kuishi kwa amani na kudumisha uiano.
Aidha mkuu huyu wa polisi katika ukanda huu ametaja kwamba pia idara ya polisi itaangazia kuwahamisha maafisa wa polisi ambao wamehudumu katika sehemu mmoja kwa kipindi cha miaka minne.
Hata hivyo Naibei ametaja kwamba oparesheni ya Ondoa majangali Marsabit iliyolenga wahalifu wa kundi la OLA imefaulu kwa asilimia kubwa.

Subscribe to eNewsletter