KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na JB Nateleng,
Wito umetolewa kwa wakazi wa Marsabit kuchukua tahadhari wanapotumia maji ya mvua ambayo yanapatikana kwenye silanga.
Kwa mujibu wa waziri wa afya kaunti ya Marsabit, Malicha Boru ni kwamba maji ya silanga sio safi na iwapo hayatatibiwa ipasavyo basi uenda ikawadhuru wakazi kiafya.
Malicha amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa amechemsha maji kabla ya kutumia ili kuepukana na magonjwa yanayotokana na kunywa maji chafu.
Waziri Malicha amewachangamoto washikadau pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali kutoa hamasa zaidi kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa maji safi kwa afya yao.
Kuhusiana na suala la ugonjwa wa Kalazaar,waziri Malicha amesema kuwa wameudhibiti ugonjwa huo huku idara hiyo ikiendela kutoa hamasa kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa kuchukua tahadhari, akihofu kuwa uenda ugonjwa huo ukaongozeka kwa sababu ya mvua inayotarajiwa kunyesha hapa jimboni.