Local Bulletins

Wahalifu 3 wezi wa mifugo wauliwa na maafisa wa polisi wadi ya Karare Marsabit huku bunduki 2 zikinaswa.

Wahalifu 3 wezi wa mifugo wauliwa na maafisa wa polisi wadi ya Karare Marsabit huku bunduki 2 zikinaswa.

 Na Caroline Waforo

Watu watatu wanaodaiwa kuwa wezi wa mifugo wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi huku bunduki mbili zikinaswa katikati ya eneo la Kiturini na Karare kaunti ya Marsabit leo Jumatatu.

Hii ni baada ya jaribio la wizi wa mifugo kutibuka.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amedokeza kuwa hiyo jana Jumapili karibia wahalifu 10 waliojihami Kwa bunduki walivamia eneo la shrine katika jaribio la wizi wa mbuzi 80.

Maafisa wa akiba NPR walimenyana na wahalifu hao na kutibua shambulizi hilo ambapo wahalifu  walifanikiwa kutoroka.

Kamanda Kimaiyo amesema kuwa Leo Jumatatu maafisa wa polisi Kwa ushirikiano na maafisa wa akiba NPR walifuata nyayo za wahalifu hao wanaoaminika kutokea kaunti ya Samburu ambapo waliwapata katikati ya eneo la Kituruni na Karare na hapo makabiliano yalizuka na kupelekea mauaji ya wahalifu watatu huku wengine wakifanikiwa kutoroka.

Maafisa walifanikiwa kunasa bunduki 2 moja aina ya AK 47 na nyingine aina ya G3 pamoja na risasi 6.

Kamanda Kimaiyo ametoa onyo Kali  kwa watu walio na nia ya kutekeleza mashambulizi ya wizi wa mifugo akisema kuwa watakabiliwa vilivyo na mkono wa sheria.

Subscribe to eNewsletter