Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
NA ISAAC WAIHENYA
Wagonjwa wanougua ugonjwa wa Kalazaah katika hospitali ya Laisamis Level 4 katika kaunti ya Marsabit wanendelea vyema.
Haya ni kwa mujibi mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo Liban Wako.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Wako ametaja kwamba tayari wagonjwa kumi wameruhusiwa kwenda nyumbani hii leo baada ya kulazwa hospitali humo na kupokea matibabu kwa muda.
Hata hivyo Wako amesema kwamba kwa sasa hali ya waliokuwa wamelazwa ipo imara huku wakiendela kupokea matibabu chini ya uangalizi wa maafisa wa afya.
Kadhalika Wako ameweka wazi kuwa bado idadi ya wanaougua maradhi hayo inazidi kuongeza huku watu 6 zaidi wakilazwa hapao jana hospitalini humo.