Local Bulletins

Wafugaji Marsabit wametakiwa kuwa tayari na dawa za kutibu magonjwa ya baridi na homa ya mifugo msimu huu wa mvua.

Na Samuel Kosgei

WAFUGAJI katika kaunti ya Marsabit haswa sehemu zinazoshuhudia mvua kwa sasa wametakiwa kuwa tayari na dawa za kutibu magonjwa ya baridi na homa ya mifugo.

Afisa wa idara ya kilimo, Saku kaunti hii ya Marsabit Dub Nura amesema kuwa wakati wa msimu wa mvua mara  nyingi mifugo haswa zile dhaifu na wale wadogo hupatwa na magonjwa ya baridi suala ambalo mkulima anafaa kujiandaa na dawa mapema.

Wakati huo amewashauri wakulima na wafugaji katika jimbo la Marsabit kukumbatia kilimo-biashara badala ya kutegemea kilimo au ufugaji pekee bila kujihusisha na shughuli nyingine za kusaka lishe na fedha.

Subscribe to eNewsletter