Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wafugaji katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuuza baadhi ya mifugo wao na kusalia na mifugo wachache ambao wataweza kumudu.
Kwa mujibu wa aliyekuwa diwani wa wadi ya North Horr Galgallo Tuye ni kuwa kwa sasa ni wakati mwafaka kwa wafugaji kuuza mifugo wao waliokatika hali nzuri ili kuepuka hasara wakati wa ukame.
Tuye aliyezungumza na idhaa hii wakati wa mafunzo ya wanakamati wa kamati za mabadiliko ya tabia nchi kutoka wadi mbalimbali za jimbo la Marsabit yanayofadhiliwa na shirika la Friends of Lake Turkana (FoLT) amesema kuwa wafugaji hapa jimboni walipata hasara kubwa wakati wa kiangazi cha kati ya mwaka wa 2021 na 2023 jambo ambalo halifai kujitokeza tena.
Aidha Tuye ametaja kwamba kando na kupoteza mifugo wafugaji pia walipitia changamoto nyingi ikiwepo magonjwa na hata mizozo kati ya jamii mbalimbali.
Kuhusiana na swala moto ambao huteketeza nyasi na kuharibu mazingira Tuye ameitaka serekali kuweka sharia kali itakayowakabili wale wanaendeleza uovu huo.