Local Bulletins

Wafanyibiashara wanne wa vileo wakamatwa mjini Marsabit kwenye oparesheni ya NACADA.

Na Joseph Muchai,

Wafanyibiashara wanne wa vileo wamekamatwa mjini Marsabit kwa kuhudumu pasipo na leseni.

Wanne hao wamekamatwa kwenye oparesheni ya kukabiliana na mihadarati iliyoendelezwa na mamlaka ya kupambana na vileo na dawa za kulevya nchini NACADA, serikali kuu na ya kaunti pamoja na mamlaka ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS.

Akuzngumza na Radio Jangwani baada ya shughuli hiyo afisaa mratibu wa NACADA Alice Mwangi amesema kwamba shughuli hiyo ambayo itaendelea kwa siku kadhaa inanuia kuhakikisha kuwa biashara ya bidhaa ghushi na dawa za kulevya inakomeshwa.

Afisaa wa mamlaka ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS Erick Karani amedhibitisha kuwa hakuna bidhaa ghushi zilizopatikana katika oparesheni ya leo ijapokuwa kreti moja ya vileo vilivyopitisha muda wake wa kutumiwa.

Subscribe to eNewsletter