Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
Wabunge kutoka maeneo kame nchini wametakiwa kushirikiana pamoja ili kusukuma uwepo wa fidia au usaidizi kwa wafugaji wanaopoteza mifugo yao kutokana na ukame katika sehemu za kiangazi.
Mshirikishi wa shirika la Friends of lake Turkana, Makambo Lotorobo ameambia shajara kuwa wabunge wa maeneo haya kupitia muungano wa wabunge wa eneo la kaskazini na maeneo kame wanafaa kuhakikisha kuwa serikali inawapa usaidizi wafugaji watakaoathirika na vifo vya mifugo.
Aidha amewataka wafugaji wenyewe kutafuta bima mifugo yao ili kuepuka hasara ya mifugo kufa kutokana na kiangazi.
Kwa upande wake aliyekuwa MCA Wa Kargi South Horr, Asunta Galgidele akizungumza kwenye kipindi cha Amkia Jangwani amewaomba akina mama kusaka mbinu nyingine ya kumudu familia bila kutegemea tu ufugaji wa mifugo kwani miaka ya leo ufugaji imetatizwa na mabadiliko ya Tabia Nchi.