Local Bulletins

Waadhirika wa virusi vya HIV Marsabit, wahofia hali yao ya afya.

Na Joseph Muchai,

Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kaunti ya Marsabit wanahofia hali yao ya afya kufuatia kuondolewa kwa msaada wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo maarufu ARV kutoka kwa shirika la misaada la Marekani USAID.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani mtetezi wa maslahi ya watu wanaoshi na virusi vya ukimwi katika kaunti ya Marsabit mwalimu Qabale Tache amesema kuwa kwa sasa hawajui hali yao itakuwaje kwani kufikia muda wa kuodoa msaada kwa nchi mbalimbali, Kenya ilikuwa na dawa za kuwamudu waadhirika wa ugonjwa huo kwa kipindi kifupi tu.

Qabale pia ameonya kuwa huenda maambukizi yakaongezeka kutokana na uhaba wa dawa hizo humu nchini.

Kwa sasa wanaomba serikali kuingilia kati na kuokoa hali haswa ikizingatiwa kuwa Wakenya wengi wanaoishi na magonjwa yanayohitaji kushughulikiwa kimatibabu kila wakati kama vile kisukari.

Ameitakaserekali kuhakiki kuwa wagonjwa wanapata dawa kwani iwapo watalazimika kununua dawa hizo basi huenda hali ikawa ngumu kutokana na bei ya juu ya dawa hizo.

Itakumbukwa kuwa serikali ya Marekani kupitia kwa rais wake Donald trump ilisitisha msaada wake kwa shirika la afya duniani WHO na pia kwa mataifa mbali mbali punde tu baada ya kuapishwa mnamo mwezi januari mwaka huu.

Subscribe to eNewsletter