Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Caroline Waforo,
Visa vya unajisi na ubakaji vinasalia kuwa kero kubwa hapa katika kaunti ya Marsabit.
Haya yamebainika wakati wa kikao cha kukusanya maoni kuhusu ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia na mauaji ya wanawake vinavyoendeshwa na jopo maalum la kuchunguza visa hivi liloloteuliwa na Rais William Ruto miezi mitatu iliyopita kufuatia ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake hapa nchini.
Kulingana na afisa wa magereza Said Shano ambaye amezungumza katika kikao hicho visa hivi ni kati ya kesi zinazowaandama wafungwa gerezani.
Aidha Shano amesema kuwa wanaotekeleza visa hivi ni watu wa karibu sana na waathiriwa.
Maeneo ya Loiyangalani na Laisamis ni kati ya maeneo yaliyoathirika pakubwa kati ya maeneo mengine jimboni.
Katika siku za hivi karibuni visa vya unajisi vimeongezeka pakubwa huku onyo likitolewa kwa wanaotekeleza unyama huo.
Katika eneo bunge la Moyale visa vya ulawiti vimeripotiwa kuongezeka.