Local Bulletins

Visa vya ugonjwa wa figo vyatajwa kuongezeka kaunti ya Marsabit huku wito wa kujipima ukitolewa.

Na JB Nateleng

Waziri wa afya kaunti ya Marsabit Malicha Boru amesema kuwa visa vya ugonjwa wa figo vinazidi kuripotiwa katika kaunti ya Marsabit.

Akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea siku ya figo duniani iliyoadhimishwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit, waziri Malicha amesema kuwa visa vya ugonjwa wa figo vinazidi kuongeza jimboni huku visa vingi vikiripotiwa katika eneo la Moyale, North horr na Saku huku akiwataka wakazi kujitokeza na kujipima hali yao ya afya.

Malicha ameelezea kwamba idara ya afya inajizatiti kuhakikisha kuwa vifaa vya kupima ugonjwa wa Figo vinapatikana kwa urahisi jimboni ili kusaidia katika kutambua ugonjwa huo mapema.

Hata hivyo amesema kuwa serekali inapanga kuogeza mashine mbili zaidi katika kituo cha figo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya kusafisha figo katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.

Kadhalika Malicha amedokeza kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit inazidi kuboresha idara ya afya kwa kuhakikisha kuwa hospitali zote za rufaa jimboni zina kituo cha figo (Renal Unit) huku wakiwa na mipango ya kufungua hospitali ya rufaa ya Sololo mwezi ujao.

Subscribe to eNewsletter