Local Bulletins

Visa vya ugonjwa kifua kikuu (TB) vyaongezeka kaunti ya Marsabit.

Na Sabalua Moses

Huku dunia ikiadhimisha siku  ya kifua kikuu (TB) duniani  msimamizi mkuu anayesimamia maswala  ya kifua kikuu katika kaunti ya Marsabit Bi Sore amesema kuwa visa vya ugonjwa huo katika kaunti ya Marsabit  vimeongezeka tangu mwaka jana, huku akiwataka wakaazi kuwa mstari wa mbele  kuenda kupimwa na kupata matibabu pindi wanapohisi joto jingi mwilini, ama kukohoa kwa sana.

Hata hivyo  Bi Sora amesema asilima 11 ya wale wameathirika na ugonjwa huo ni watoto huku  akiwahakikishia wagonjwa kuwa idara yake imeimarisha  dawa za  kupambana na ugonjwa huo wa kifua kikuu.

 Aidha, Bi Sora amesema kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa kifua kikuu ni ukosefu  wa lishe bora pamoja na ukosefu  wa hewa safi manyumbani.

Vile vile Bi sora amewataka wakaazi kuwaacha unyanyapaa kwa wagonjwa  hao akisema TB  ina tiba.

Wakati huo huu Bi sora ameitaka serikali ya kaunti ya Marsabit pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kusaidia katika kupambana na makali ya ugonjwa huo wa kifua kikuu huku akiwahakishia wagonjwa usalama wao hata baada ya kusitishwa kwa msaada wa shirika la kimarakeni USAID.

Subscribe to eNewsletter