KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Mwandishi Wetu
WAKAAZI wa eneo la Songa eneobunge la Saku kaunti hii ya marsabit wameombwa kushirikiana na asasi za usalama ili kukomesha visa vya ubakaji vinavyodaiwa kufanyika katika eneo hilo siku za hivi maajuzi.
Akizungumza na kituo hiki naibu chifu wa songa Luka Lolkipayangi ameomba wananchi waliona na taarifa zitakazosaidia kukamatwa mshukiwa wa ubakaji wa mtoto wa miaka aliyefanya kitendo hicho na kutoroka kusikojulikana.
Mshukiwa dali parsole anadaiwa kumnajisi mtoto msichana wa miaka sita katika eneo la songa na kutoroka wiki jana.
Chifu Luka amesema kuwa mshukiwa huyo angali anatafutwa na pindi atakapokamatwa atashtakiwa na kwa makosa anayodaiwa kuyafanya.
Huku akikemea unyama huo chief Luka ameahidi kuwa mshukiwa atakamatwa kwani mkono wa serikali ni mrefu.
Amesema kuwa kuna haja ya jamii kushirikiana na idara ya usalama kukomesha matumizi ya dawa za kulevya ambayo anataja kuwa ndio chanzo kikuu cha kujitokeza kwa visa hivyo vya ubakaji.