KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Viongozi wa chama cha ODM katika kaunti ya Marsabit wametetea hatua ya kinara wa chama hicho Raila Odinga kufanya kazi na Rais Wiliam Ruto wakiitaja hatua hiyo kama ya kizalendo na wala sio Handsheki.
Wakizungumza wakati wa zoezi la kuwasajili wanachama wapya lililoandaliwa hapa mjini Marsabit, viongozi hao wakiogozwa na MCA wa Hellu Manyataa Siba Haila Michael,wamesema kuwa hatua ya Raila ililenga kutuliza joto la kisiasa ambalo lilikuwa likipanda hapa nchini.
Aidha MCA Siba amewata viongozi ambao tayari wameaza siasa za mwaka wa 2027 kusitisha na badala yake kuangazia kuwafanyia wananchi kazi ili kuleta maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Marsabit Alinur Mumin amewasuta wale wanaoitaja hatua ya Raila kama usaliti huku akitaja kama iliyo na nia ya kuhakikisha kwamba serekali inatimiza ahadi zake ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za mwaka wa 2022.
Vilevile viongozi hao wametoa wito kwa wananchi kujisajili ili kukipa chama hicho nguvu wakati wa uchanguzi mkuu ujao.
Kauli zao zilishabikiwa pia na mwanachama wa kamati ya uchaguzi ya chama cha ODM anayewakilisha makundi maalum Bi. Halima Daro ambaye ameitaja hatua ya Raila na Rais Ruto kuungana kama jambo bora kwa taifa la Kenya.