Local Bulletins

Viongozi wa kisiasa watakiwa kuheshimu sehemu za dini kwa kujiepusha na siasa kanisani.

Na Joseph Muchai

Huku hisia mseto zikiendelea kuibuliwa kwenye sehemu mbali mbali za nchi kuhusiana na siasa kanisani. Wanasiasa wametakiwa kukoma kufanya siasa kanisani na kuheshimu madhabahu.

Mchungaji wa kanisa la KAG Marsabit ambaye pia ni mwanachama katika muungano wa wachungaji katika kaunti ya Marsabit Joseph Mwenda amewataka viongozi wanasiasa kuheshimu kanisa na kujitenga na siasa kanisani.

Akiongea na idhaa hii mchungaji mwenda amesema kuwa kila jambo linafaa kufuata utaratibu wake kwani kila jambo lina wakati wake. Amewataka kutofautisha wakati wa ibada na wakati wa siasa.

Aidha amewataka wanasiasa kutambua kuwa watu wanaohudhuria kanisa ni wa kutoka maeneo mbali mbali na  mirengo mbalimbali ya kisiasa na hivyo kuheshimu swala hilo.

Na kuhusiana ana kutangaza kiwango cha pesa wanazotoa wanasiasa, Mwenda alikuwa na haya ya kusema

Wakaazi katika kaunti ya Marsbit pia hawakukosa la kusema kuhusiana na hilo. Baadhi yao wanasema kuwa sio vyema kwa wanasiasa kufanya siasa kanisani. Hata hivyo wengi wanahisi kuwa hawafai kukatazwa kuongea wala kutoa pesa kanisani.

Wengini pia wameelezea kuwa kanisani ni mahali patakatifu na hivyo basi haifai kutumika kwa mambo yasiofaa.

Haya yanajiri siku kadhaa baada ya kanisa la Kiangilikana (ACK) kupitia askofu wake mkuu Josphat Ole Sapit kupiga marufuku wanasiasa kupatiwa nafasi ya kuongea kanisani akihoji kuwa kanisani sio mahali pa kupigia siasa. Aidha alishtumu wanasiasa kwa kutoa pesa kanisani kwa kujionesha, akihoji kuwa matoleo kanisani sio nafasi ya watu kujionesha au kujigamba.

Subscribe to eNewsletter