Diocese of Marsabit, Local Bulletins

VIJANA WA KANISA LA KIANGILIKANA KAUNTI YA MARSABIT, WARAI VIJANA NCHINI KUTOKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA KUVURUGA AMANI.

Picha Hisani

Na Joseph Muchai,

Viongozi wa vijana kutoka Parokia mbalimbali za kanisa la kiangilikana la ACK daosisi ya Marsabit wameelezea uwezo wa vijana kuboresha uongozi wa nchi siku za usoni.

Wakizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani vijana hao wameonesha imani yao kuwa vijana wana uwezo wa kubadilisha siasa na uongozi wa siku za usoni.

Vijana hao wameonya dhidi ya viongozi kuwatumia vijana kwa njia isiyofaa kwani huleta mathara.

Viongozi hao wa vijana wanahisi kuwa iwapo vijana watatambuliwa huenda wakaleta mabadiliko makubwa huku wakiirai serekali kuwashirikisha vijana katika maswala ya uongozi na wala sio sauti zao kuzimwa au malalamiko yao kufumbiwa macho.

Wakati uo huo vijana hawa wamekariri haja ya kuzingatia sauti ya vijana kama njia mojapo ya kuboresha uongozi wa nchi na huduma kwa wananchi.

Subscribe to eNewsletter