Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Moses Sabalua,
Kufuatia ongezeko la matumizi ya akili mneba almaarufu AI viongozi wa kidini katika kaaunti ya Marsabit wamewataka vijana haswa kuonyesha maadili mema wanapotumia mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kasisi katika kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG) hapa mjini Marsabit Joseph Mwendwa, amesema kwamba kuwepo kwa teknelojia hiyo kumewasidia watoto pamoja na vijana katika masomo yao na kuifanya hata kuwa rahisi.
Wakati uo huo Kasisi Mwendwa amesema kwamba teknolojia hiyo pia ina madhara kwani watu wengi hubakia kuwa wavivu kwani teknolojia hiyo ya akili mnemba inawasaidia katika kufanya kazi hizo kwa urahisi.
Vile vile kasisi Mwendwa amewataka vijana kutumia miundo mIsingi yenye maadili mema wanapotumia mitandao ya kijamii ili kuweza kubadilisha maisha ya wanachi.