KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Samuel Kosgei
HUKU dunia ikiadhimisha siku ya kulala duniani, wito wa kupata usingizi wa kutosha umetolewa kwa wakaazi wa Marsabit ikitajwa kama njia moja ya kupunguza msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa afya ya akili katika hospitali kuu ya Marsabit Victor Karani ameambia shajara ya jangwani kuwa mtu mzima anafaa kulala pahali safi na sehemu ambayo haina usumbufu wa haina yoyote ikiwemo kelele.
Karani ameongeza kuwa kinywaji ambacho mtu anakunywa au kula kabla ya kulala ni muhimu sana ikizingatiwa kuwa baadhi ya vinywaji kama vile kahawa na vilivyo na vyenye kafein vinaondoa usingizi hivyo haifai endapo mtu anapanga kulala.
Muda wa saa sita hadi nane anasema ndio mwafaka kwa mtu mzima kulala.
Aidha daktari Karani anasema kuwa usingizi wa kutosha una umuhimu sana kwa afya ya akili ya binadamu kwani usingizi ni mbinu moja ya kudhibiti msongo wa mawazo.
Anasema kuwa mtu aliyetosheka usingizi huwa amechangamka na hupata suluhu ya shida kwa haraka kinyume na asiyepata usingizi wa kutosha.
Siku ya Kulala Duniani iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na Jumuiya ya Kulala Duniani, ambayo hapo awali ilijulikana kama Chama cha Kimataifa cha Tiba ya Usingizi (WASM).