Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
MWAKILISHI wadi wa Sololo John Boru ameonesha wasiwasi wake kutokana na hali ya kiangazi kuwa mbaya katika wadi yake suala analosema linahatarisha maisha wakaazi kutokana na ukosefu wa chakula na maji.
MCA Boru akizungumza na kituo hiki ofisini mwake amesema kuwa idadi kubwa ya watu hawana uwezo wa kupata chakula labda kupitia msaada kidogo wa mashirika au kupitia serikali kuu, chakula anachosema ni kidogo.
Kwenye suala la maji anasema kuwa ofisi yake imetembelea idara ya maji ya Marsabit ili kushughulikia kuharibika kwa visima vinavyotegemewa na wananchi.
Licha ya kusema kuwa msaada kidogo wa chakula huwafikia wakati mwingine kutoka serikali ya kitaifa bado kuna haja ya watu hao kusaidiwa na mashirika ya kibinafsi na hata kupitia mkono wa kaunti.
Kisima kilicho eneo la Anona anasema kuwa kilibahati kuwa na maji na hivyo wanasubiri ripoti ya idara ya maji kabla ya kushughulikiwa kwa kisima hicho.
Boru anasema kuwa hali hiyo imechangiwa sana na mvua kidogo kushuhudiwa msimu uliopita na pia athari za ukame ulioshuhudiwa miaka miwili iliyopita ambapo mifugo mingi ilikuwa.
Amesema kuwa kuna haja ya uongozi wa serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuwekeza fedha kwenye suala la uzalishaji wa chakula na maji ili kuepuka kutegemea msaada wa mataifa ya kigeni ambayo kwa sasa yamekatisha misaada yao.