Local Bulletins

Ukosefu wa ajira wasababisha ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia kaunti ya Marsabit.

Na JB Nateleng,

Visa vya ukosefu wa ajira sawa na utepetevu kwenye malezi vimetajwa kama chanzo kukuu cha ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia katika kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la MWADO mwanaharakati Nuria Gollo ni kwamba iwapo vijana watakosa kujukumishwa basi huenda wakawa na fikira mbaya ambazo zinawafanya kujiingiza katika utumizi wa mihadarati n ahata kufanya vitendo vinavyoathiri wanajamii.

Nuria ameeleza kwamba licha ya vijana kujulikana kuwa na nguvu ya kufanya kazi ambayo italeta maendeleo bado kuna haja ya kutoa hamasa kwao juu ya vile watajukumika katika ujenzi wa taifa.

Kuhusiana na suala la visa vya ubakaji kuongezeka katika eneo la Songa, Nuria amesema kuwa jamii ya Songa inafaa kushirikiana na asasi za usalama ili kuwakamata wale ambao wanatelekeza uovu huo.

Mwanaharakati huyu amenyoshea kidole cha lawama wale ambao wanaficha wahusika wa dhulma za kijinsia akisema kuwa chuma chao ki motoni kwani ndio wanaorejesha jamii nyuma katika vita dhidi ya dhulma za kijinsia.

Subscribe to eNewsletter