Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
NA SAMUEL KOSGEI.
Wanaume kaunti hii ya Marsabit na sehemu mbali mbali nchini wametakiwa kusaka usaidizi wa afya ya akili pindi wanapopitia magumu maishani kwani ndio njia kuu ya kupata suluhu ya msongo wa mawazo.
Daktari wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Victor Karani amesema kuwa wanaume wanafaa kuhusishwa kwenye mazungumzo na mijadala ya afya ya akili kwani mara kwa mara wamesahaulika kwenye mazungumzo hayo.
Amewarai wanaume kusaka usaidizi pindi wanapopitia ugumu maishani bila kuogopa kwani wengi huchukulia kuwa kusema matatizo yako ni ishara ya udhaifu kama jamii nyingi nchini inavyochukulia.
Aidha amewataka familia au marafiki ya wanaume walio na mawazo mengi kujaribu kuzugunguza nao badala ya kuwapuuza.
Katika mwezi huu wa kutoa hamasisho kuhusu afya ya akili kwa wanaume na wavulana, Dkt karani amesema mengi yanafaa kufanywa kwani hamna hamasisho ya kutosha kuhusu msongo wa mawazo ambayo wanaumme wanapitia nchini ikilinganishwa na wanawake.
Anasema kuwa kuna haja ya uwepo wa wataalamu wengi haswa katika kaunti ya Marsabit ambao wataisaidia kusuluhisha shida ya afya ya akili.
Dr. Karani amezidi kusema kuwa taaluma anayofanya mtu pia kwa upana mara nyingi huchangia kutulia kiakili au kupata matatizo ya afya ya akili labda kupitia ugumu wa kazi na mshahara mdogo.
Mahusiano kwenye ndoa, mizozo ya kifamilia na ugumu wa uchumi pia ni swala ambalo anasema wanaume wanakapitia na huchangia msongo wa mawazo.