Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Henry Khoyan
Mkurugenzi na mtafiti katika shirika la utafiti wa kilimo na mifugo (KALRO) hapa Marsabit, Qabale Diba Badake, ametoa wito kwa wakulima na wafugaji kuendelea na juhudi zao katika sekta ya kilimo na ufugaji licha ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Akizungumza katika hafla ya Siku ya kuadhimisha wiki utafiti yaani KALRO Research Week hapa Marsabit siku ya Alhamisi, Qabale amesema kuwa shirika hilo limejitahidi kuleta mabadiliko makubwa katika sekta hizo, lakini bado kuna vikwazo vinavyohitaji kushughulikiwa.
Amesema kwamba changamoto zipo, lakini ni muhimu kwa wakulima na wafugaji wasife moyo kwani Mabadiliko yanawezekana.
Kaimu mkurugenzi wa Shirika la hilo la (KALRO), Yusuf Ali, ametaja maendeleo mapya katika uzalishaji wa mmea wa Teff. Amesema kwamba shirika hilo limekuja na aina mpya ya mbegu za teff zenye uwezo mkubwa wa kuvuna, ikilinganishwa na mbegu zilizokuwa zikitumika na wakulima hapa Marsabit hapo awali ambazo hazikuwa na ubora mzuri.
Mbegu hizo mpya, kutoka KALRO, zimeimarishwa ili kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mavuno bora zaidi.
Ali amesisitiza umuhimu wa kutumia mbegu hizo bora katika kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima hapa Marsabit.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo na Mifugo katika shirika la (KALRO) amewasihi wakulima na wafugaji kuendelea kutembelea shirika hilo ili kupata maarifa na ujuzi wa kisasa katika shughuli zao za ukulima na ufugaji.
Aidha, ameweka rasmi kwamba katika siku zijazo, shirika hilo litakuwa likisambaza mbegu za kupanda kwa wafugaji katika kaunti ya Marsabit na kaunti jirani kama vile Mandera na Wajir.