Local Bulletins

Sherehe ya siku ya wanyamapori ulimwenguni yaadhimishwa  mjini Marsabit na shirika la KWS

Na Moses Sabalua.

Huku ulimwengu ukisheherekea siku ya wanyamapori duniani  shirika la kulinda wanyamapori KWS mjini Marsabit walijumuika pamoja na washikadau mbali mbali katika kuadhimisha siku hiyo katika kaunti ya marsabit hii leo.

Akizungungumza na wanahabari  mjini marsabit Msimamizi mkuu wa  KWS Agostin Ajuoga amesema kuwa lengo kuu la siku hii ni kuwekeza katika  jamii   kwani kuna umuhimu wa kulinda   wanyama pori ikizingatiwa ina manufaa kwa jamii pakubwa pamoja na nchi kwa jumla.

Vile vile Justin Aoga amesema ni sharti jamii ielewe umuhimu wa wanyamapori pamoja na misitu huku akiwataka jamii katika kaunti ya Marsabit kuwa mstari  wa mbele kulinda misitu pamoja na wanyamapori.

Aidha Ajuoga ameitaka jamii  inaoishi  pamoja  na wanyamapori  kufahamu umuhimu wa kuwatunza wanyamapori  hao  na  vile vile kutafuta namna ya kujisajili kama maeneo ya kuwahifadhi hao wanyama.

Wakati uo huo Ajuoga  ameaomba washikadau mbali mbali kushirikiana kwa pamoja ili kusaidia jamii katika kulinda wanyamapori katika kaunti ya Marsabit huku akiwataka walioathiriwa na wanyamapori kuripoti kesi  za  mashambulizi ya  wanyamapori kwa shirika hilo la KWS.

Subscribe to eNewsletter