Local Bulletins

Serikali ya Kenya na ile ya Ethiopia zaanza mchakato wa kutafuta amani ya kudumu mpakani.

Na Caroline Waforo,

Serikali za nchi za Kenya na Ethiopia kwa pamoja zimeanza mchakato wa kutafuta amani ya kudumu mpakani kufuatia matukio ya utovu wa usalama ya hivi maajuzi ambapo kijana moja raia wa Kenya aliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Dukana eneo bunge la North Horr kaunti ya Marsabit huku nao watu watatu raia wa Ethiopia wakiuuawa nchini humo na wanne wakijeruhiwa ikiaminika ni kisa cha kulipiza kisasi.

Katika mkutano wa amani ulioandaliwa katika eneo la Moyale Custom upande wa Ethiopia hii leo na kuleta pamoja idara za serikali kutika mataifa yote mawili, kamati ya usalama katika jimbo la Marsabit, wazee wa jamii husika jimboni Marsabit na taifa jirani la Ethiopia, imebainika kuwa hali ya uhasama miongoni mwa jamii katika maeneo ya mipakani imechangiwa na wahalifu.

Serikali ya Kenya na jamii imepewa jukumu la kuwasaka wahalifu waliotekeleza mauaji ya raia wa Ethiopia kulingana na mkataba wa maelewano katika ya Mikona Dillo inayofahamika kama Maikona Dillo Declaration.

Hii ni baada ya upande wa Ethiopia kusema kuwa tayari washukiwa watatu wamekamatwa wakihusishwa na mauaji ya raia wa Kenya.

Akizungumza katika mkutano huo naibu mwenyekiti wa kamati ya amani jimboni Marsabit Adan Chukulisa amesema kuwa jamii hizo mbili zitahakikisha kuwa amani inapatikana.

Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amewapa wazee wa jamii muda wa wiki moja kufanya mazunguzmo na jamii husika ili kupata suluhu la changamoto zilizopo haswa katika maeneo ya mipakani.

Kadhalika ametoa onyo kali kwa wanaoeneza uvumizi na propaganda ambazo zinaweza kuchangia uhasama miongoni mwa jamii mbalimbali akisema kuwa watachukuliwa hatua za kisheria

Subscribe to eNewsletter