Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Samuel Kosgei
Serikali ya kaunti ya Marsabit imeirai shule zote za upili na zile za kiufundi ambazo zina wanafunzi wanaopokea ufadhili kutoka serikali ya kaunti kuendelea kuvumilia na kutofukuza wanafunzi hao hadi mzozo uliopo utakapotatuliwa.
Kwenye barua kwa vyombo vya habari na kwa shule mbali mbali zilizo na wanafunzi wanaofadhili na kaunti msemaji wa kaunti Abdub Barilleh amesema kuwa serikali zote za kaunti nchini zipo kwenye harakati ya kuweka sahihi makubaliano na wizara ya elimu wiki hii hatua anayosema itatatua mzozo uliokuwepo kati ya ofisi ya mdhibiti wa bajeti na baraza la magavana COG.
Kuchelewa kutumwa kwa pesa hizo shuleni kulisababishwa na marufuku iliyowekwa na ofisi ya mkaguzi wa bajeti suala lililochochea magavana kuelekea mahakamani na kushinda kesi hiyo kwenye maamuzi yaliyofanywa tarehe 8/4/2025 jijini Nakuru.
Kulingana na barua iliyotiwa sahihi na Barille serikali ya kaunti ya Marsabit kwa sasa inalipia karo wanafunzi 4,568.