Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Ebinet Apiyo
Ombi limetolewa kwa serikali ya kaunti ya Marsabit kuongeza idadi ya vizoa uchafu mtaani Marsabit ili kuhakikisha usafi wa mazingira ndani na nje ya mitaa.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake Mkurugenzi wa mazingira katika shirika la NEMA, Naphtali Osoro ameomba serikali ya kaunti ya Marsabit kuongeza idadi ya vizoa uchafu kufuatia madai ya kuwa takataka zinatupwa ovyovyo mjini haswa kwenye mikondo ya maji au kwenye madaraja.
Vilevile afisa Osoro ametoa wito kwa wananchi kuweza kuzingatia sheria za mazingira wanapotupa uchafu kwani ni jukumu la kila mmoja kutunza mazingira na iwapo mtu yeyote atakwenda kinyume na sheria ya mazingira atajipata taabani.