Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na JB Nateleng,
Ipo haja ya serekali ya kaunti ya Marsabit kuangazia masuala ya elimu ya chekechea (ECDE) katika eneo la Loiyangalani.
Haya ni kwa mujibu wa msimamizi wa shirika la World Vision eneo la Loiyangalani Jarso James.
Akizungumza kwenye kongomano lililowaleta pamoja washikadau wa elimu kutoka idara ya elimu kaunti ya Marsabit, pamoja na wawakilishi wadi ambayo ilifadhiliwa na shirika la World Vision, Jarso amesema kuwa watoto katika eneo la Loiyangalani wanapitia changamoto nyingi katiak kusaka elimu ya chekechea.
Jarso amesema kuwa watoto wengi wanakosa kuenda shule kwa sababu ya kutokuwa na madarasa ya kutosha pamoja na walimu wa kuwafunza huku akiwarai washikadau kuungana ili kutatu kero hilo.
Jarso ameitaka idara ya elimu kaunti ya Marsabit kuweza kuwaajiri walimu bila kuegemea eneo, kabila ama mrengo wa kisiasa akisema kuwa kuna maeneo ambayo yanahitaji wa walimu zaidi na yanafaa kupewa kipau mbele katika zoezi la kuwaajiri walimu.
Vilevile ameitaka serekali ya Marsabit kuangazia masuala ya afya katika eneo la Loiyangalani akisema kuwa afya ya watoto pamoja na watu wazima ambao wanaishi fora inazidi kuzoroteka.
Kando na hilo Jarso ameweka wazi kuwa shirika la World Vision lipo tayari kusaidia katika kuinua hadhi ya elimu katika maeneo kame jimboni kwa manufaa ya wanajamii.