Local Bulletins

Serekali ya kaunti ya Marsabit imekataa kutulipa mishahara yetu na inatuzungusha tu. – Interns wa Marsabit walalama.

Na Isaac Waihenya,

Wanafunzi wa nyajani maarufu Intern katika kaunti ya Marsabit wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kuhangaishwa na serekali ya kaunti na kudinda kuwalipa mishahara yao baada ya wao kukamilisha kipindi chao cha kuhudumu.

Wakizungumza na Shajara na Radio ya Radio Jangwani kwa njia ya simu wanafunzi hao wakiongozwa na Mohamed Waqo kutoka Moyale wamelalama kuwa idara ya fedha jimboni Marsabit imewkuwa ikiwazungusha na kudai kwamba haijapa orodha kamili ya wanafunzi wanaofaa kulipwa, huku idara ya elimu ikitaja kwamba iliwasilisha orodha hiyo mnamo mwezi Septemba mwaka jana.

Waqo ameweka wazi kwamba bado kuna wanafunzi ambao wanadai serekali ya kaunti mishahara ya miezi mitano, wengine miezi minne huku wengine wakiidai serekali ya kaunti mishahara ya miezi mitatu.

Waqo imeitaka kamati ya elimu katika bunge la kaunti ya Marsabit sawa na kamati ya Utawala kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba wanapata mishahara yao.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya elimu katika kaunti ya Marsabit Josphine Leado kwenye mazungumzo na meza ya habari ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya simu ameweka wazi kuwa kamati hiyo itaandaa kikao na waziri wa elimu katika kaunti ya Marsabit sawa na washikadau wengine husika ili kuweza kupata suluhu la kero hilo.

Leado ameahidi kutoa maelezo zaidi kuhusiana na swala hilo pamoja na kuchelewashwa kwa karo za wanafunzi wanaofadhiliwa na serekali ya kaunti ya Marsabit baada ya kukamilika kwa mkao kati ya kamati ya elimu na waziri wa elimu hapo kesho.

Subscribe to eNewsletter